Luke 18:15-17

15 aPia, watu walikuwa wakimletea Isa watoto wachanga ili awaguse. Wanafunzi wake walipoona hivyo, wakawakemea. 16 bLakini Isa akawaita wale watoto waje kwake, akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. 17 cAmin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”

Mtawala Tajiri

(Mathayo 19:16-30; Marko 10:17-31)

Copyright information for SwhKC